AFYA YAKO KWANZA

JE UNATAKA USHAURI AU DAWA ZA ASILI PIGA 0763371047

Sunday, July 14, 2019

Faida tano za kutumia Mlonge

 Tokeo la picha la faida za mlonge
Moringa maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.

Hizi ndiyo faida za mmea huo ambao unatibu maradhi mbalimbali:
1. Mti wa Mlonge husaidia watu walioathilika kiongeza cd4 cell (white blood cell) ndani ya mwili wa binadamu ambayo humsaidia mgonjwa kuondokana na miwasho katika damu na kuupa mwili nguvu na kuongeza hamu ya kula
2. Mti wa Mlonge hutibu maradhi sugu kama vile Kisukali (Kuimalisha na kurekebisha viwango ya sukari katika umri wa mwanadamu), Pressure, malaria, homa ya mara kwa mala, Saratani ya tumbo, hupunguza sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji, jambo amabalo ni adimu kwa watu wengi pia huondoa uchovu mwili na kukufanya uwe na afya nzuli, mchangamfu na mwenye furaha
3. Majani na maua ya Moringa yanavirutubisho vingi kama vitamin A ( mara tatu zaidi ya karoti), Vitamini C (mara tatu zaidi ya ile ya machungwa), calcium (mara 140 zaidi ya ile inayopatikana katika maziwa ya gombe) na Potasiamu. Mmea huu umetumika kusadia udhibiti wa matatanisho yanayoletwa na ugonjwa wa ukimwi.
4. Faida nyingine itokanayo na unga wa majani ya mti wa mlonge ni kusafishia maji ambayo ni machafu na kuweza kuwa safi na salama na kuwa tayari kwa matumizi yoyote ya nyumbani kama vile kupikia na kunywa hii inaweza kuwa ni mbadala ya madawa mengine yanayoweza kutibu maji kama vile watergard na mengineyo.
5. Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi. Waweza kutumia majani kama unavyotumia mchaichai na hapo unatibu homa. Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi (zingatia usikaushe kwenye JUA)​Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
Zipo faida nyingi za mmea huu ambao umegeuka kimbilio kwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment