
Majani ya mpera yana faida kiafya kama tunda la pera. Majani ya mpera yana virutubisho vya kuzuia uvumbe na tannins zinafaida nyingi kiafya ikiwemo kutibu maumivu ya tumbo pamoja na ugonjwa au magonjwa ya kansa.
Faida ya majani ya mpera ni kama yafuatayo;
KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI
- Matumizi ya majani ya mpera husaidia kupunguza kiwango cha madhara kwa binadamu. Matumizi ya majani ya mapera yanaweza kusaidia kuepuka matatizo ya magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.
KUHARISHA
- Tafiti za kisayansi zimeonyesha kuwa kunywa chai ya majani ya mpera huweza kusaidia kukomesha tatizo la kuharisha
SARATANI YA TEZI DUME
- Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Iycopene ambayo ni muhimu katika kupambana na saratani ya tezi dume kwa kuzuia uzalishaji wa homoni aina ya adrogen ambayo ni chanzo cha ukuaji wa chembe za saratani ya tezi dume
KUPUNGUZA UZITO
- Virutubisho vilivyoko kwenye jani la mpera husaidia kupunguza uzito kwa kuzuia wanga kuwa sukari ambapo mageuzo ya wanga kuwa sukari husababisha ongezeko la uzito kwenye mwili wa binadamu
No comments:
Post a Comment